Nina manahodha saba kikosini - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Nov 2020
Nina manahodha saba kikosini - Sven

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ametolea ufafanuzi wa uamuzi wake wa kubadili nahodha wa kikosi chake kwenye baadhi ya mechi

Katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Jonas Mkude ndiye aliyakabidhiwa kitambaa cha unahodha

Wapo walioona mabadiliko hayo kama jambo linaloashiria sintofahamu kwani katika mchezo huo, nahodha msaidizi Mohammed Hussein alikuwepo dimbani

Hata hivyo Sven amesema anao wachezaji saba kwenye kikosi chake ambao anaweza kuwatumia kama manahodha na hivyo sio ajabu kumkabidhi kitambaa mchezaji mwingine nje ya wale wanaofahamika

"Tuna wachezaji zaidi ya saba ambao wanaweza kuvaa kitambaa cha unahodha. Ni suala la kawaida kubadilisha manahodha kulingana na mechi," amesema Sven

Ufafanuzi kama huo ulitolewa hivi karibuni na Msemaji wa Simba Haji Manara ambaye alisisitiza kuwa ni uamuzi wa kocha kumkabidhi kitambaa cha unahodha mchezaji yeyote katika kikosi cha Simba lakini inafahamika nahodha ni John Bocco na Msaidizi ni Zimbwe Jr

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’