Ndemla anawanyamazisha wakosoaji wake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Nov 2020
Ndemla anawanyamazisha wakosoaji wake

Kuna wakati yalisemwa mengi sana kuhusu kiungo Said Khamis Ndemla. Wapo waliojaribu kumvuruga wakati wa usajili wakitaka asiongeze mkataba na Simba kwa kuwa hapati nafasi ya kucheza

Lakini pia uongozi wa Simba ulimuongeza mkataba mpya wengine wakahoji wanamuongezea mkataba wa nini wakati hatumiki?

Aidha Ndemla mwenyewe akasisitiza kutokuwa na mpango wa kuondoka Simba akiamini kuwa nafasi yake ipo

Ubora huja kwa muda lakini kipaji ni kipo tu, ndivyo ilivyokuwa kwa Ndemla

Sasa amekuwa kwenye kiwango cha juu sana, Etienne Ndayiragie, hakufanya makosa kumjumuisha kwenye kikosi chake cha timu ya taifa

Ndemla amefunga mabao mawili katika mechi mbili zilizopita. Lakini ni mchezaji aliyeimarika sana na umuhimu wake unaonekana kwenye kikosi cha Sven Vandenbroeck

Wakati huu anafanya vizuri, hutawasikia wale waliokuwa wakimbeza na kukosoa uwepo wake katika klabu ya Simba

Simba iliona mbali kumuongeza mkataba, kwani wanafahamu uwezo wake. Ndemla yuko kwenye kikosi cha Simba kwa zaidi ya miaka nane

Amelelewa Msimbazi na huu ni wakati wake wa kulipa fadhila kwa Wanamsimbazi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’