Waamuzi sita kusimamia dabi Jumamosi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Nov 2020
Waamuzi sita kusimamia dabi Jumamosi

Bodi ya ligi imebainisha kuwa waamuzi sita watatumika kwenye mchezo wa kwanza wa watani wa jadi msimu huu kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, Novemba 07 uwanja wa Taifa

Kuanzia msimu uliopita, TFF imeweka utaratibu wa kutumia waamuzi sita kwenye mchezo unaozikutanisha Yanga na Simba

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo amesema lengo la kutumia waamuzi sita ni kupunguza makosa na kuongeza umakini

Bado Bodi ya Ligi haijaweka hadharani majina ya waamuzi hao lakini zipo taarifa za kuwa wanaweza kuwa Martin Saanya, Ramadhan Kayoko, Abdallah Mwinyimkuu, Selemani Nonga na Abdulaziz Ally

Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mchezo huo wa kwanza msimu huu ambao awali ulipangwa kupigwa Oktoba 18 lakini ukasogezwa mbele

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa nusu fainali michuano ya kombe la FA msimu uliopita, Simba ikifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 4-1

Katika msimu huo, Simba na Yanga zilikutana mara tatu, matokeo ya sare ya mabao 2-2 yalipatikana kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kabla ya Yanga kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa mzunguuko wa pili

Lakini Simba ikadhihirisha umwamba wake katika nusu fainali ya FA kwa ushindi wa mabao 4-1

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’