Ushindi mwingine wa kibabe ulioambatana na 'pira biriani' wameupata Simba leo dimba la Uhuru wakiipeleka puta Kagera Sugar na kuichapa mabao 2-0
John Bocco na Said Khamis Ndemla wameihakikishia Simba alama tatu muhimu leo, Bocco akianza kufunga kupitia mkwaju wa penati kabla ya Ndemla kufunga bao lake la pili katika mchezo wa pili mfululizo

Ulikuwa mchezo ambao kiurahisi Simba ingeweza kushinda sio chini ya mabao matano, kama washambuliaji wake wangekuwa makini
Clatous Chotta Chama 'CCC' maarufu mwamba wa Lusaka, vyovyote wasemavyo huyu mtu mpira anaujua
Kuna kila sababu ya Simba kumuhitaji katika kikosi kwenye kila mchezo, awapo uwanjani maisha yanakuwa rahisi sana
Wenyewe wanasema leo walikuwa mazoezini tu, mechi itapigwa Jumamosi Novemba 07 pale dimba la Taifa watakapowakabili watani zao Yanga
Hii Simba hii, weka mbali na watoto...!