Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameeleza kufurahishwa na kuimarika viwango vya wachezaji Ibrahim Ajibu na Said Ndemla ambao walifunga mabao kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui Fc
Sven amesema nyota hao wameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao wanapopata nafasi na hivyo kumfanya aendelee kuwa na imani kuwa kikosi chake kitaendelea kutamba licha ya changamoto ya majeruhi iliyowakabili washambuliaji wake muhimu hivi karibuni
Ajibu na Ndemla walifunga mabao wakati Simba ikishinda mechi yake ya ligi kuu mbele ya Mwadui FC kwa mabao 5-0 katika Uwanja wa Uhuru, Dar juzi Jumamosi. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na John Bocco aliyefunga mawili na Hassan Dilunga.
Sven amesema kuwa kitendo cha wachezaji hao kufunga kinampa wigo wa kuona wana uwezo wa kupata mabao na pointi kwenye mechi yoyote

"Kila mmoja anaweza kufunga mabao hapa wala siyo kuwategemea Bocco, Kagere au Mugalu pekee. Ndemla, Dilunga wamefunga, ni jambo zuri na hii inafanya tuwe na mifumo mingi ya kucheza na tukapata mabao"
"Kocha anaweza kumpenda mshambuliaji anayefunga mabao 15 kwa msimu lakini siku ambayo akikamatwa na wapinzani timu haitafunga, hivyo kwa namna hii ya kila mtu kufunga inanifanya niwe na mbinu mbadala za kupata pointi," alisema Sven
Leo Simba itakuwa na kibarua kingine uwanja wa Uhuru itakapoikabili Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri