Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba jioni ya leo watashuka uwanja wa Uhuru kupepetana na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kupata ushindi mnono katika mchezo uliopita kwa kuibugiza Mwadui Fc mabao 5-0, vijana wa Sven Vandenbroeck wamepania kuendeleza wimbi la ushindi leo dhidi ya Kagera Sugar ambayo huwa hawatabiriki kila wanapokutana na Simba
Mchezo huu unapigwa siku tatu kabla ya mchezo wa kwanza wa dabi msimu huu dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi Novemba 07 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Simba inahitaji kuondoka na alama zote tatu ili kupunguza tofauti ya pointi baina yake na washindani wake Azam Fc na Yanga
Viingilio vya mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri, VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-