Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere jana alianza mazoezi mepesi akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda ambayo inajiandaa na mechi za kufuzu michuano ya Afcon 2021 zitakazopigwa wiki ijayo
Kagere alipewa ruhusa na uongozi wa Simba kurejea kwao Rwanda kutibu majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania
Matibabu yake yanasimamiwa na mtaalam wake ambaye pia ndiye daktari wa timu ya Taifa ya Rwanda
Pamoja na kocha Sven Vandenbroeck kusema kuwa mfungaji bora huyo wa ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo kuwa anaweza kukaa nje kwa wiki tatu, llolote linaweza kutokea Jumamosi, Novemba 07 pale dimba la Mkapa!
ADVERTISE HERE