Kulingana na takwimu zilizotolewa na gazeti la Champion, beki kisiki wa Simba Asante Kwasi ndiye mchezaji wa mwisho kuifunga Simba mwezi Novemba mwaka jana kabla haijamsajili.
Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 41 baada ya kucheza michezo 17 bila ya kupoteza mchezo hata mmoja. Ndio timu pekee inayoshikilia rekodi hiyo msimu huu.
Wakati akichezea Lipuli FC, beki Asante Kwasi alifunga bao pekee la Lipuli kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Hiyo ilikuwa Novemba, 26, mwaka 2017.
Baada ya hapo, Simba imecheza michezo sita bila kuruhusu bao hata moja ambapo imecheza dhidi ya Ndanda FC (2-0), Singida United (4-0), Kagera Sugar (0-2), Majimaji (4-0), Ruvu Shooting (3-0) na juzi dhidi ya Azam FC (1-0).

ADVERTISE HERE