Mwezi huu wa tano, mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Simba watashuka dimbani mara tano, mechi mbili zikiwa za nyumbani na tatu ugenini
Mchezo wa kwanza wa nyumbani utapigwa keshokutwa Jumatano dhidi ya Kagera na kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Yanga Novemba 07
Baada ya mchezo dhidi ya Yanga ligi itasimama kwa wiki mbili kupisha kalenda ya michezo ya kuwania kufuzu michuano ya AFCON 2021 Tanzania ikisafiri nchini Tunisia
Novemba 21 Simba itakuwa ugenini mkoani Tanga kuumana na Coastal Union na baadae kusafiri jijini Dodoma kuikabili Dodoma Jiji Novemba 24
Novemba 29 Simba itarudi jijini Dar es salaam kuikabili kMC
ADVERTISE HERE