Wakati kukiwa na matumaini kwa washambuliaji Meddie Kagere na Chris Mugalu kurejea uwanjani mapema, kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kiungo raia wa Brazil Gerson Fraga anaweza kuwa nje kwa muda mrefu
Sven amesema Fraga atakuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa baada ya kubain jeraha alilopata litahitaji matibabu zaidi
"Meddie Kagere na Mugalu wanaweza kurejea mapema. Kagere anaweza kuwa tayari baada ya wiki moja au mbili, Mugalu madaktari wanamuangalia. Fraga tunaweza kumkosa kwa muda mrefu zaidi," amesema Sven
Baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui Fc jana, kikosi cha Sven kitacheza na Kagera Sugar kabla ya mchezo dhidi ya Yanga wiki ijayo
ADVERTISE HERE