Baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui Fc jana, mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba watarejea tena uwanja wa Uhuru siku ya Jumatano kuikabili Kagera Sugar
Mchezo huu utakuwa sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa uwanja wa Mkapa Novemba 07
Ushindi mnono waliopata dhidi ya Mwadui Fc umerudisha ari na morali ya wachezaji kuelekea mtanange huo wa Jumatano
Aidha kurejea kikosi kwa Clatous Chama, imekuwa 'boost' kubwa, sasa ni mwendo wa vipigo tu kila ajae mbele
ADVERTISE HERE