Nahodha wa Simba John Bocco ameendelea kujiongezea rekodi katika ligi ya soka Tanzania Bara baada ya jana kuwasaidia mabingwa hao wa nchi kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui Fc
Ni katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Uhuru, Simba ikirejesha utamaduni wake wa kugawa vipigo vikali
Bocco alifunga mabao mawili katika mchezo huo, na hivyo kufikisha mabao matatu msimu huu
Aidha mshambuliaji huyo mkongwe amejiongezea takwimu zake za muda wote sasa akifikisha mabao 129
Ndiye anayeshikiria rekodi ya ufungaji bora wa muda wote
ADVERTISE HERE