Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, Simba leo imemaliza hasira zake kwa Mwadui Fc baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Vijana wa Sven Vandenbroeck walionekana mapema tu kuwa na jambo lao, iliwachukua takribani dakika 25 kupata bao la kuongoza lililofungwa na nahodha John Bocco
Mvua ya mabao iliongezeka baada ya mapumziko, Bocco akiongeza bao la pili huku mabao mengine yakifungwa na Ibrahim Ajib, Hassan Dilunga na Said Ndemla
Ushindi huu ulisubiriwa kwa hamu na mashabiki, ni ushindi mzuri ambao umerejesha ari na morali ya wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa wiki ijayo
ADVERTISE HERE