Ni Jumapili hii pale uwanja wa Taifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Feb 2018
Ni Jumapili hii pale uwanja wa Taifa
Baada ya kukosa kushiriki michuano ya Kimataifa kwa takribani miaka mitano, Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba keshokutwa Jumapili, February 11 watashuka kwenye uwanja wa Taifa kumenyana na Gendarmarie kutoka Djibout kwenye mchezo wa kwanza kombe la Shirikisho hatua ya awali.

Mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na moja ya vikosi bora ilivyowahi kuwa navyo katika Historia yake.

Wapo wanaoiona Simba ya mwaka huu kuwa na kila dalili ya kurudia kile ilichofanya mwaka 1993 kwa kushiriki fainali ya kombe la washindi la CAF.

Aidha Simba inaanza kampeni ya michuano hiyo ikiwa na moja wa wakufunzi bora wa soka barani Afrika, Pierre Lechantre.

Kocha huyu aliwahi kuiongoza timu ya Taifa ya Cameroon kutwaa ubingwa wa AFCON mwaka 2000.

Lechantre na benchi lake la Ufundi wameahidi kuhakikisha Simba inatinga hatua ya makundi ya michuano hii ambayo mshindi wake anazoa mapesa ya kutosha!

Simba inashuka dimbani keshokutwa ikiwa bado ya moto hasa kutokana na mafanikio yake katika ligi.

Kikosi cha Simba kimeshinda michezo sita mfululizo ya ligi kuu ya Vodacom bila ya kuruhusu bao langoni mwake.

Hivyo hivyo washambuliaji wake wamefungwa jumla ya mabao 39 na kuwaacha mbali wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa wa VPL, Yanga, Azam FC na Singida United.

Viingilo vya mchezo huo tayari vimewekwa hadharani. Huu sio mchezo wa kukosa!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’