Umoja ndio silaha yetu Simba - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Oct 2020
Umoja ndio silaha yetu Simba - Manara

Pamoja na kupoteza mechi mbili zilizopita, Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema bado anaamini wana kikosi imara kinachoweza kushinda ubingwa msimu huu

Mhamasishaji huyo namba moja wa Simba amewataka mashabiki kusahau matokeo hayo yaliyopita na kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao katika mchezo dhidi ya Mwadui ambao utapigwa kesho Jumamosi

Manara amesema Simba imejiwekea malengo ya kushinda mataji hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zote zinazokuja mbele yao

"Sina shaka kuhusu hili, Simba itatatwaa ubingwa kwa msimu wa 2020/21 lakini lazima tupate matokeo mazuri ambayo yatatupa pointi tatu muhimu. Kushindwa kwetu kwenye mechi zilizopita kunaleta maumivu lakini ni muhimu mashabiki wetu wajue kwamba tunahitaji umoja kwani katika umoja wetu Simba hatujawahi kushindwa"

"Tuwaunge mkono wachezaji wetu kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc. Tuonyeshe kuwa pamoja nao, itawaongezea hamasa na inshallah tutapata matokeo," alisema Manara

Mchezo dhidi ya Mwadui Fc utapigwa Jumamosi, kuanzia saa kumi Alasiri kwenye uwanja wa Uhuru

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
47m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’