Okwi afunguka ufalme wake wa Dar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
9 Feb 2018
Okwi afunguka ufalme wake wa Dar
Mshambuliaji Emanuel Okwi ndiye kinara wa mabao ligi kuu ya Vodacom mpaka sasa akiwa ametupia jumla ya mabao 13.

Yeye pamoja na nahodha wa Simba John Bocco wameifungia timu hiyo iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi mabao 22.

Licha ya mafanikio yake msimu huu, wapo wanaohoji kwa nini amekuwa hafungi timu yake inapocheza nje ya jiji la Dar es salaam.

Okwi amesema haoni kama hilo ni tatizo. Kwani jambo la msingi zaidi ni yeye kufunga kuisaidia timu yake na haijalishi anafunga kwenye uwanja gani.

"Jambo la msingi hapa mimi najitahidi kufunga kila ninapopata nafasi," amesema Okwi katika mahojiano na mtandao mmoja wa michezo.

"Hata mikoani huwa napata nafasi lakini bado sijafanikiwa kuzitumia lakini ninapocheza uwanja wa Uhuru/Taifa ninapata nafasi na nazitumia kufunga."

"Hivyo ninaweza kufunga mahali popote muhimu ni kuzitumia nafasi zinazopatikana"

Aidha Okwi alizungumzia maisha yake ya soka la Kimataifa alipokwenda kucheza Etoile Du Sahel ya Tunisia na baadae kutimkia Denmark ambapo alieleza sababu zilizomuondoa kwenye timu hizo.

"Nina sababu ya msingi ya kutaka kuwa wakala wa wachezaji nikimaliza kucheza kwani ningependa sana vilabu vyetu vya Afrika Mashariki viwaandae wachezaji kwa ajili ya kuvuka level fulani.

"Ukiangalia level ya mpira wa Tanzania na Tunisia au Denmark ni tofauti sana. Kuna sababu kadhaa ambazo zilinitoa Tunisia pia kuna sababu zilizonitoa Denmark.”

“Tunisia ilikuwa ni sababu za kiuchumi, Etoile du Sahel kipindi hicho haikuwa kwenye nafasi nzuri ya kulipa mishahara ya wachezaji, ukiangalia kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na madai kwenye klabu na wengi waliondoka, mimi walishindwa kunilipa kwa zaidi ya miezi mitatu kwa hiyo tukavunja mkataba nikarudi Uganda baadae nikaja Yanga.”

“Wakati naenda Denmark tayari nilikuwa najitambua na niliamini nitafanya vizuri kwa sababu ilikuwa nafasi kubwa ya kucheza Ulaya lakini kwa bahati mbaya mambo hayakuwa kama nilivyopanga. Sikupata nafasi sana lakini ukiangalia katika mwaka mmoja na nusu sikucheza hata asilimia tano ya michezo klabu kwa hiyo tukakaa na uongozi wa timu tukafikia makubaliano kwamba hakuna faida kwa kila upande.”

“Mimi kama mchezaji haiwezekani niendelee kukaa kwa sababu sikuwa nafaidika kwa chochote nikapoteza nafasi hadi timu ya taifa na kupoteza kujiamini kwa upande wa klabu wakawa hawawezi kuendelea tena kunilipa mshahara.”

“Timu za taifa na vilabu zinatakiwa kuangalia soka kuanzia chini kabisa kwa ajili ya kuwaweka tayari wachezaji kucheza level nyingine. Kuwajenga kinidhamu, technical na tactics kwa sababu mpira wa Ulaya upo tactical sana tofauti na sisi huku lakini huku hatufuatilii sana nidhamu ya mchezo.”

“Nilipofika Denmark kocha alikuwa nanisisitiza sana nicheze namba tisa lakini ukiangalia umbo langu na wachezaji wa Denmark walivyo ni warefu sana na wananguvu halafu ni nchi ambayo system yao iko tactical sana kwa hiyo nikashindwa kuingia kwenye mfumo wa kocha na yeye hakuwa tayari kubadili mfumo kwa ajili ya mtu mmoja.”

“Ni lazima tuwaandae wachezaji wetu wa baadaye tuhakikishe wanafanikiwa zaidi yetu sisi," alisisitiza Okwi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5m ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →