Lile jinamizi ya majeruhi Simba limeanza kuachia baada ya wachezaji waliokuwa na majeraha kuanza kurejea kikosini
Nahodha John Bocco juzi alirejea mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, na jana beki Ibrahim Ame naye akarejea
Ame alikosekana tangu aliposhiriki mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Fc
Mpaka sasa wachezaji ambao bado wanatajwa kuwa majeruhi ni washambuliaji Meddie Kagere, Chris Mugalu na kiungo Gerson Fraga kukiwa na matumaini kuwa nao watarejea mapema
Jumamosi Simba itashuka tena uwanja wa Uhuru kumenyana na Mwadui Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom raundi ya nane
Mchezo huu ni wa kufa au kupona kwa Simba, kwani baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, hakuna matokeo ambayo mashabiki watayapokea zaidi ya ushindi
ADVERTISE HERE