Nahodha wa Simba John Bocco kwa niaba ya wachezaji, amewaomba radhi mashabiki baada ya timu kupoteza mechi mbili mfululizo
"Wanachama viongozi pamoja na wapenzi wote wa Simba sc kwanza nimshukuru mungu kwa kuwapa moyo wa upendo wana simba wote wakuipenda timu yetu na kuiunga mkono katika vipindi tofauti na kila mkoa tunaokwenda kuchez"
"Kwa niaba ya wachezaji niseme tunaomba mtusamehe kwa matokeo tuliyopata ya michezo yote miwili iliyopita, tuliteleza na tumeshateleza hatupaswi kuteleza tena na hii ndio ahadi yetu kwenu"
"Tutarekebisha makosa yetu na kurudi kwenye sura mpya na upambanaji mpya kwa michezo yote ijayo ili turudishe furaha yetu kwakupata motokeo mazuri kama tulivyozoea"
"Tumesha waangusha tunakiri hili ila tunaamini hali hii haitajitokeza tena kwa michezo ijayo"
SIMBA NGUVU MOJA