Manara asisitiza Umoja Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Oct 2020
Manara asisitiza Umoja Simba

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewapa pole mashabiki baada ya timu yao kupoteza mechi mbili mfululizo ligi kuu ya Vodacom

Manara amesema hiki ni kipindi kigumu kwa mashabiki wote wa Simba lakini hawana namna kwa kuwa wakati mwingine ndivyo mpira ulivyo, wanapaswa kuendelea kuwa wamoja

"Kwanza nitoe pole sana kwa matokeo mabaya mfululizo tuliyoyapata kwenye michezo yetu miwili mfululizo. "Haya sio mazoea yetu,sio Simba tunayoitaka sisi,lakini ndio ukatili wa huu mchezo ulivyo na kiukweli hatuna budi kukubali yaliyotokea!

"Ndugu zangu najua inauma sana, lakini Simba ni klabu yetu na hatuna klabu nyingine tuipendayo toka moyoni zaidi ya hii. "Inaweza kufikirisha kidogo Kama tunaweza kurudi katika nguvu yetu, lakini mimi Haji Manara nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba msimu huu hatutachukua ubingwa.

"Muhimu ni kujikosoa pale ambapo labda tunadhani tunateleza na kutorudia makosa ( Kama yapo) Ila mimi narejea kuwaambia inaweza kuwa upepo wa ukatili wa mchezo wenyewe wa mpira,ukizingatia katika mechi zote mbili tulipoteza nafasi kadhaa za kuweza kupata matokeo tofauti na tuliyoyapata!

"Kitu cha kufanya katika kipindi hiki kigumu kwetu ni kuwa na utulivu na kuwa wamoja, namaanisha UMOJA. "Always (mara zote) Simba ikiwa MOJA huwa haishindwi hivi.

"Na kwa nini nasisitiza hili la UMOJA, hili tumeliandika katika mioyo yetu kama kauli mbiu yetu kuwa Simba Nguvu Moja, tukiliacha, hatujawahi kuwa Simba SC.

"Nimalizie kwa kuwaambia hiki ni kipindi mtacharurwa sana mitandaoni, maofisini na majumbani pamoja na vijiweni kwenu, ichukulieni hyo ndio raha na karaha ya football, isiwasambue hata kama itawaumiza. Naamini soon (karibuni) itageuka kwao, hatujalala ndugu zangu na hatutalala!

"Mimi mitandao yote naona kama imenielemea binafsi lakini nipo strong (imara) na bado imani yangu kuhusu Marathon hii ndefu ni kwamba tunakwenda kuchukua ubingwa wa nne mfululizo. Inshaallah."

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’