Sven ana maswali ya kuwajibu mabosi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Oct 2020
Sven ana maswali ya kuwajibu mabosi Simba

Kufungwa mechi mbili mfululizo kwa klabu kubwa kama Simba ni matokeo yasiyokubalika. Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ana maswali ya kuwajibu mabosi wake kutokana na matokeo haya

Simba ina wachezaji wengi mahiri, kukosekana kwa Chama, Kagere au Mugalu haiwezi kuwa sababu ya timu kufungwa kizembe

Bado naamini Simba ina kikosi bora sana ukilinganisha na timu nyingine hata inapowakosa wachezaji hao

Simba itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu, mechi za hatua ya awali zikitarajiwa kupigwa mwezi ujao

Sio kwa Simba hii ya Sven ambayo inapungua makali siku hadi siku. Sven ana kazi ya kufanya kuhakikisha anarejesha makali ya timu kabla ya kuanza kwa michuano hiyo

Suala la upangaji wa kikosi bado linaonekana kuwa changamoto kwake. Wachezaji wengine wametumika sana huku wengine wakiwa na nafasi finyu kikosini, matokeo yake wengi wamepoteza kujiamini na sasa madhara yake yanaonekana

Ni jambo la hatari kama inafikia wakati timu haiwezi kupata matokeo kama mchezaji mmoja au wawili wanakosekana

Pamoja na kuwa na wachezaji mahiri, Sven amepoteza ile dhana ya Simba kuwa na kikosi kipana, kwani jambo hilo halionekani tena

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’