Tutashinda mechi 20 mfululizo ligi kuu - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Oct 2020
Tutashinda mechi 20 mfululizo ligi kuu - Manara

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na hofu ju ya timu yao kwani mkakati wao ni kushinda ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo

Manara amesema kupoteza mchezo sio jambo la kuwakatisha tamaa kwani hutokea kila msimu lakini muhimu ni zile hesabu za mwisho baada ya msimu kukamilika

"Mwaka juzi tulipoteza na Mbao katika raundi za mwanzo mwanzo za ligi kuu kule Mwanza, nakumbuka hadi chupa za maji tulirushiwa pale kirumba

"Halikadhalika msimu uliopita tulifungwa na Mwadui mwanzoni kabisa mwa msimu, tukaaambiwa tunaachia ubingwa. Mwisho wa msimu tukawa bingwa kwa tofauti ya pointi ambazo ni rekodi ya Tanzania!

"Nini maana yangu? Tunakwenda kushinda game ishirini mfululizo za ligi kuu kutokea Jumatatu, baada ya hizo game tutapiga hesabu zetu vizuri kabisa! Sure yangu ni kwamba tutakuwa Bingwa wa taifa hili hadi 2028, halafu tutaamua tufanyaje?," ametamba Manara

Kesho Jumatatu Simba itashuka uwanja wa Uhuru kumenyana na Ruvu Shooting

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’