Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba leo kinarejea 'mzigoni' kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wanahitaji kuwapa furaha mashabiki wao kwa kushinda mchezo dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kuwa wamepoteza mchezo uliopita
Aidha winga Bernard Morrison amesema watakuwa na nafasi ya kusahihisha makosa yaliyopelekea wapoteze mchezo uliopita ili kuhakikisha wanashinda mchezo wa kesho
"Tumerudi kufanyia kazi makosa yetu na kujiandaa na mchezo ujao. Mashabiki lazima wawe upande wetu sababu tutajituma na kuhakikisha kila jambo linakuwa sawa," amesema Morrison
Kikosi cha Simba kesho kinaweza kupata huduma ya nyota wake wawili Clatous Chama na Paschal Wawa ambao walikuwa miongoni mwa nyota waliokosa mchezo uliopita wakiwa nje ya nchi kushughulikia pasi zao kusafiria
Β