Wakati nahodha John Bocco akiendelea kurejea kikosini taratibu baada ya kuanza mazoezi mepesi, nyota wengine majeruhi bado wanaweza kukosekana mchezo wa Jumatatu dhidi ya Ruvu Shooting
Wakati huu Simba inapitia changamoto ya aina yake kutokana na wachezaji wake muhimu kukumbwa na majeruhi
Mpaka sasa wachezaji watano wa kikosi cha kwanza wanaendelea na program za kutibiwa majeraha yanayowasumbua
Gerson Fraga, Meddie Kagere, Chris Mugalu, Bocco na Shomari Kapombe wote wanakabiliwa na changamoto hiyo
Ni mtihani kwa kocha Sven Vandenbroeck kwani timu inakabiliwa na ratiba ngumu na muhimu zaidi ni mchezo wa Novemba 07 dhidi ya Yanga
Imeelezwa Kagere anaweza kuwa nje hadi wiki tatu wakati Mugalu, Fraga, Kapombe na Bocco wao wanaweza kurejea uwanjani mapema