Siku ya leo haikuwa upande wetu - Barbara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Oct 2020
Siku ya leo haikuwa upande wetu - Barbara

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amewataka Wanamsimbazi kukubali matokeo ambayo timu yao imepata leo mkoani Rukwa kwani ni sahemu ya mchezo

Barbara amesema ligi ina ushindani, hakuna timu dhaifu na kila timu inapambana kusaka alama tatu

Amewataka Wanamsimbazi kusonga mbele, kwa ajili ya mechi zinazofuata

"Hakuna timu dhaifu. Alimradi inashiriki VPL, basi ni timu nzuri. Leo haikua siku yetu. Tusonge mbele Wanasimba," aliandika Barbara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Simba imepoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu kwa kufungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons

Makosa ya safu ya ulinzi pamoja na mlinda lango yalipelekea Samson Mbangula kufunga bao la kichwa kupitia mpira ambao haukuwa ukionekana kuwa na madhara makubwa

Manula alipiga hesabu zake vibaya kwa kujaribu kuutokea mpira huo kabla ya kuishia njiani huku walinzi wakishindwa kuruka na Mbangula

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’