Sisi ni mabingwa, tukadhihirishe Nelson Mandela - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Oct 2020
Sisi ni mabingwa, tukadhihirishe Nelson Mandela - Manara

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema leo wachezaji wa Simba watakuwa na kazi moja tu, kuhakikisha wanapamba kupata ushindi dhidi ya Prisons

Manara amesema michezo dhidi ya Prisons katika misimu ya hivi karibuni imekuwa migumu kutokana na timu hizo kukamiana

Hata hivyo, Simba wakiwa mabingwa, wakimiliki kikosi bora zaidi nchini, wana kila sababu ya kudhihirisha kwa nini walishinda mataji yote msimu uliopita

"Prisons ni timu ngumu miongoni mwa timu ngumu katika ligi kuu ya Tanzania hususan unapokutana nao kwenye uwanja mgumu kama tunaocheza nao leo lakini Simba ni Bingwa wa taifa hili na always Bingwa hufanya vizuri popote pale"

"Mchezo dhidi ya Prisons wachezaji wetu lazma watoe jasho jingi na wapambane kweli kweli ili kupata matokeo chanya. Ligi ni ngumu ila wao ni wachezaji bora kabisa. Insha'Allah kwa juhudi zao na maarifa ya makocha wetu, na kwa Dua na Sala zetu Wanasimba Insha'Allah tutashinda pale Nelson Mandela Stadium," aliandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’