Prisons vs Simba, mechi ya kibabe Sumbawanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Oct 2020
Prisons vs Simba, mechi ya kibabe Sumbawanga

Mabingwa wa nchi Simba leo wako mkoani Rukwa ambapo saa kumi jioni watakuwa na kibarua cha kuwakabili maafande wa Tanzania Prisons katika mchezo utakaorindima uwanja wa Nelson Mandela

Huu ni mchezo ambao unakwenda kudhihirisha ile dhana ya kuwa na kikosi kipana kwani pamoja na kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu wa kikosiΒ  cha kwanza, kocha Sven Vandenbroeck amesema Prisons wasubiri sapraizi kutoka kwa mabingwa

Sven amesema timu yake itakuwa na mabadiliko ya kimbinu, amewasoma Tanzania Prisons hivyo leo anaamini wana kila sababu ya kupata ushindi

Ni mchezo ambao utapigwa katika mazingira ya viwanja ambavyo sio rafiki kwa soka kutembea chini, lakini Simba hii tayari imedhihirisha viwanja hivyo sio tatizo kabisa

Pale mkoani Dodoma JKT Tanzania walikuwa 4-0 katika uwanja wa Jamhuri ukipigwa mpira wa kiwango cha 'kutisha'

Ni mchezo ambao Simba inahitaji kushinda ili kuendelea kubaki nafasi ya pili kuipa presha Azam Fc iliyoanza vyema msimu kwa kushinda mechi zao zote

Mabadiliko makubwa yanayotarajiwa kwenye kikosi ni kwenye safu ya ushambuliaji baada ya John Bocco na Meddie Kagere wote kukosekana kutokana na majeraha

Lakini pia, eneo la kiungo Clatous Chama hatakuwepo na kwenye ulinzi Paschal Wawa nae hatakuwepo

Mzee wa kuwakeraaa Bernard Morrison leo anaweza kuanzishwa kama mshambuliaji pacha na Chris Mugalu huku Francis Kahata akiwa na nafasi ya kurejea kikosini kama ilivyo kwa Hassan Dilunga na Miraji Athumani 'Sheva'

Kennedy Juma anaweza kurejea katika safu ya ulinzi lakini pia Sven anaweza kumtumia Erasto Nyoni ambaye alijumuishwa katika kikosi kilichotua Sumbawanga juzi jioni

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’