Meneja wa klabu ya Simba Patrick Rweyemamu amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa kesho Alhamisi kwenye uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga
Simba iliwasili Sumbawanga jana wakitokea mkoani Mbeya ambako waliweka kambi ya muda mfupi kujiandaa na mchezo huo
Rweyemamu amesema timu inakamilisha maandalizi ya mwisho jioni ya leo kwenye uwanja wa Nelson Mandela
"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho kama tunavyofanya kwa michezo yote. Leo tutafanya maandalizi ya mwisho kwenye uwanja tutakaocheza kesho
"Tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tunaamini kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tunahitaji pointi tatu muhimu ili kuendelea kuyafuata malengo yetu tuliyojiwekea ya kutwaa ubingwa," amesema
Hii ni mara ya pili Simba inacheza Sumbawanga mwaka huu. Mwanzoni mwa mwezi August walicheza mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Namungo Fc na wakafanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0