Majeruhi Simba waanza mazoezi, Niyonzima kutibiwa India

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Feb 2018
Majeruhi Simba waanza mazoezi, Niyonzima kutibiwa India
Maandalizi ya kikosi cha Simba kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya awali dhidi ya Gendarmarie yanaendelea vizuri kulingana na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Manara amesema baada ya ushindi dhidi ya Azam FC jana na kujikita kileleni kwa tofauti ya alama saba, kikosi cha Simba kiko kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Gendarmarie utakaopigwa Jumapili Februari 11 kwenye uwanja wa Taifa.

Wakati huo huo Manara amesema kiungo fundi Haruna Niyonzima anatarajia kusafiri wakati wowote kwenda India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye mguu, na kwamba haitachukua zaidi ya wiki mbili atakuwa amerejea uwanjani.

Manara amesema wachezaji wengine ambao walikuwa na majeraha wameanza kurejea kwenye mazoezi ya pamoja na timu.

Said Mohamed 'Nduda' ameshaanza mazoezi huku Salim Mbonde akitarajiwa kujiunga mazoezini wakati wowote baada ya kumaliza program ya gym na beach.

Aidha kwa kuwa Simba na Yanga zote zina majukumu ya kuliwakilisha Taifa wikiendi hii kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la ligi ya mabingwa, Manara amewataka mashabiki wa Simba watakaokwenda uwanja kutazama mchezo wa Yanga kutozomea.

"Natoa wito kwa washabiki wa Simba watakaoenda uwanjani kwenye mechi ya Yanga Jmosi wasiizomee,tuzomeane kwenye ligi ya nyumbani kwani sisi sote ni Watanzania na tunawakilisha nchi moja," amesema Manara
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’