Chama anaamini Simba itafanya makubwa Ligi ya Mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Oct 2020
Chama anaamini Simba itafanya makubwa Ligi ya Mabingwa

Kiungo fundi wa Simba, Clatous Chama ana matumaini makubwa ya timu yao kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Novemba 20, mwaka huu ambapo michezo ya hatua ya awali itapigwa. Kwa msimu wa 2020/21, Simba ndiyo wawakilishi pekee wa michuano hiyo hapa Tanzania

Akizungumzia nafasi ya Simba kwenye michuano hiyo, Chama amesema kwa usajili makini uliofanyika, matumaini ni makubwa msimu huu wanaweza kufika mbali

"Nawapongeza viongozi kwa kufanya usajili bora, ukiachana na mashindano mengine tutakayoshiriki, tunafahamu tuna kibarua cha Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Zimebaki siku chache kabla ya kuanza michuano hiyo, naona kila mchezaji hapa anajitahidi kuboresha kiwango chake ili kuingia kwenye kikosi cha kwanza. Naamini ubora wa kikosi cha msimu huu na funzo la kuaga mashindano mapema msimu uliopita ni vitu vitakavyotufanya tufanye vizuri," amesema Chama

Simba ilitwaa ubingwa msimu wa 2019/20 jambo linalowapa nafasi ya kushiriki michuano mikubwa Afrika ya Ligi ya Mabingwa inayowahusisha mabingwa wa ligi za timu za Afrika

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’