Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema amefurahishwa na kasi ya Chris Mugalu ya kucheka na nyavu, lakini pia akieleza atalazimika kubadilisha mfumo kuelekea mechi dhidi ya Tanzania Prisons ambayo itachezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Alhamisi wiki hii
Juzi Mugalualifunga mabao mawili dakika ya nane na 68 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mlandege kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam huku bao lingine likifungwa na Ame Ali dakika ya 16, na la wapinzani Yahya Haji akilitupia dakika ya 72.
Sven amesema Mugalu amekuwa kaikat kiwango kizuri na ana imani ataisadia timu hiyo kupata idadi ya kubwa ya mabao kwenye mechi za Ligi Kuu.
Kuhusu mechi dhidi ya Prisons, Sven alisema mechi za ugenini ni tofauti na wanapocheza nyumbani hali ambayo itamlazimu kuhakikisha anabadili mfumo kulingana na uwanja pamoja na mpinzani wao.
"Mechi ya ugenini kwetu ni ngumu, iwe tunacheza na timu yoyote ile, tofauti na tunapocheza nyumbani, nategemea kubadilisha mfumo kulingana na mpinzani, ila siwezi kuweka wazi juu ya mfumo nitakaotumia," alisema
Simba iko mkoani Mbeya ambako imeweka kambi ya muda mfupi kabla ya kuelekea Rukwa tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Alhamisi