Okwi, Ndemla, Kichuya wamkuna Lechantre

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
8 Feb 2018
Okwi, Ndemla, Kichuya wamkuna Lechantre
Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba wameshaanza mipango mikakati ya kuwakabili wapinzani wao Gendarmerie kutoka nchini Djibouti ili watoke na ushindi na tayari Kocha Mkuu wake, Pierre Lechantre amewapa shavu la maana nyota wake watatu.

Mfaransa huyo alisema Said Ndemla, Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi na kama watacheza vizuri katika michuano hiyo ya kimataifa ni rahisi kwao kupata timu nje ya nchi na kucheza soka la kulipwa hasa Ulaya kwani ni wakali kinoma kwa soka yao.

Lechantre alisema kila kitu ni ndoto kama wachezaji hao wakiwa na ndoto ya kutamani kwenda mbele zaidi kwa muda aliokaa ndani ya Simba ana imani wanaweza na wakalifanikisha hilo haswa kupitia haya mashindano ya Kimataifa ambayo yanafuatiliwa na timu nyingi kubwa Afrika hata Ulaya.

“Kila kitu ni ndoto siwezi kuzungumzia kwa upande wao lakini nimewaona wana uwezo na wakijituma katika michuano ya CAF wanaweza kwenda mbali zaidi kisoka,” alisema.

“Tangu nimefika Simba nimekutana na wachezaji wote wana vipaji vya hali ya juu jambo ambalo litanifanya kutofanya kazi katika mazingira magumu na kunipa matumaini kuwa naweza kufanya vizuri kwa kushirikiana nao,” alisema Lechantre.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
19h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE →