Mshambuliaji Chris Mugalu leo ameendeleza mwenendo wa kuzifumania nyavu baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 ambao Simba imepata dhidi ya Mlandege Fc
Ni katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Azam Complex jioni ya leo
Mugalu sasa amefunga katika kila mchezo aliocheza tangu atue kwa mabingwa hao wa nchi
Amefikisha mabao saba. Bao la tatu katika mchezo huo lilifungwa na beki Ibrahim Ame
Huyu ndio mshambuliaji sasa, wala hakupokelewa kwa mbwembwe JNIA
ADVERTISE HERE