Mabingwa wa Taifa hili Simba jioni ya leo majira ya saa 11 watashuka kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi kucheza na Mlandege Fc ukiwa ni mchezo wa kirafiki
Wiki hii Simba haina majukumu kwenye ligi hivyo uongozi wa wababe hao wa soka nchini wakaona si vibaya kuwapa burudani mashabiki wao kwa kujipima nguvu dhidi ya Mlandege kutoka visiwani Zanzibar
Hii inaweza kuwa shoo nyingine ya mshambuliaji Christ Mugalu ambaye moto wake wa kuzifumainia nyavu hauzimiki
Mugalu amefunga kwenye kila mchezo ambao amecheza
Leo anaweza kuongoza safu ya ushambuliaji baada ya John Bocco kuwa majeruhi huku MK 14 Meddie Kagere akichelewa kurejea kutoka majukumu ya timu ya Taifa
Bila shaka leo mvua haitawaharibia burudani mashabiki wa Simba kwani mapema wiki hii Simba ilifuta mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Ndanda Fc kutokana na changamoto ya mvua