Manara awapa Yanga nafasi ya tatu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2020
Manara awapa Yanga nafasi ya tatu

Baada ya Klabu ya Azam FC kuwa na muendelezo mzuri kwenye Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu huu, msemaji wa Simba Haji Manara amesema wanaweza kushika nafasi ya pili nyuma yao huku akiwatabiria watani zao Yanga kumaliza katika nafasi ya tatu msimu huu

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amewapongeza Azam Fc kwa kuunda kikosi cha ushindani msimu huu

"Kwa mwenendo huu naiona Azam Fc ikipigania taji msimu huu, mna kikosi kizuri na kwakweli mnastahili hongera.Timu inayopigania mataji huwa hailalamiki lalamiki hovyo, huwaoni na makabrasha TFF wala FIFA au CAS"

"Hamkupokea mchezaji kwa mbwembwe bandarini wala stendi ya Ubungo lakini manonesha mlivyodhamiria"

"Najua msimu huu mtakamata nafasi ya pili nyuma ya championi wa Taifa hili, yule wa tatu mtamuacha kwa pointi ishirini na tano," alichagiza Manara

Ushindi wa Azam umewafanya wafikishe alama 18 katika mechi 6 walizocheza msimu huu na wametengeneza tofauti ya alama 5 na vilabu kongwe na mabingwa mara nyingi wa ligi hiyo Simba na Yanga wenye alama 13

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
21h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’