Azam Fc wanaweza kuwa washindani msimu huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2020
Azam Fc wanaweza kuwa washindani msimu huu

Wakati mabingwa wa nchi Simba wakitarajia kucheza mchezo wao wa sita ligi kuu ya Vodacom Jumatano ijayo dhidi ya Tanzania Prisons, wana rambaramba Azam Fc wanaonekana kuanza msimu kibabe baada ya jana tena kuifunga Mwadui Fc mabao 3-0

Ushindi huo unaifanya Azam Fc iweze kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi zao zote

Mshambuliaji wao Prince Dube ndiye kinara wa mabao kwenye ligi akiwa amefunga mabao sita

Huyu jamaa anaonekana kuwa hatari kwani amehusika katika mabao tisa, kafunga sita katengeneza matatu ndani ya mechi sita

Pengine hawa Azam Fc wanaweza kuwapa changamoto Simba msimu huu katika kuwania ubingwa

Hata hivyo ni pale watakapocheza na Mnyama ndio itafahamika kama ni washindani au ni moto wa kifuu tu

Kuongezeka kwa ushindani ni dhahiri kutainufaisha Simba inayokabiliwa na majukumu ya michuano ya ligi ya mabingwa baadae mwezi ujao

Simba imeziacha mbali sana kwa ubora timu nyingi zinazoshiriki ligi kuu. Mabingwa hao wa nchi hawapati ushindani ule ambao wataenda kukutana nao kule katika ligi ya mabingwa

Kuimarika kwa Azam kutamuongezea nidhamu kocha Sven Vandenbroeck katika maandalizi ya kikosi chake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
31m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’