Jumapili, Februari 11, 2018 kikosi cha Simba kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili klabu ya Gendarmarie kutoka nchini Djibout katika mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho hatua ya awali.
Gendarmarie ilianzishwa mwaka 2002 na ni moja ya timu zinazofanya vizuri katika ligi kuu ya nchini Djibout.
Msimu uliopita ilimaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Klabu hiyo iko imara kiuchumi kwani ina uwanja wake unaochukua takribani watazamaji 40,000.
Licha ya kutokuwa na jina kubwa kwenye ramani ya soka barani Afrika, Simba itafaa kuivaa timu hiyo kwa tahadhari kubwa.
Ili kuhakikishia inasonga mbele lazima Simba ipate ushindi mnono katika mchezo wa kwanza unaopigwa katika ardhi ya nyumbani.
Tayari kikosi cha Simba kimeanza maandalizi kuelekea mchezo huo baada ya jana kuichapa Azam FC bao 1-0.
Aidha uwepo wa kocha Pierre Lechantre katika michuano ya Kimataifa utainufaisha Simba kuelekea mchezo huo.
Moja ya malengo ya kikosi cha Simba ni kuhakikisha inatinga hatua ya makundi kwenye michuano hiyo namba mbili kwa ukubwa baada ya ile ya ligi ya mabingwa.

ADVERTISE HERE