Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo baada ya mapumziko ya mechi za Kimataifa
Mechi za raundi ya sita zinaanza kupigwa leo ambapo mechi nne zitachezwa katika viwanja mbalimbali
Mkoani Dodoma, JKT Tanzania iliyotoka kufumuliwa mabao 4-0 na Simba kwenye mchezo uliopita, itakuwa nyumbani ikiikaribisha Ruvu Shooting mchezo ukitarajiwa kupigwa saa nane mchana
Michezo mingine ni kati ya Biashara United dhidi ya Ihefu, KMC dhidi ya Coastal Union na Namungo Fc dhidi ya Kagera Sugar
Mabingwa wa nchi Simba wao hawatakuwa na mchezo wiki hii baada ya mchezo wao dhidi ya Yanga kuahirishwa
Watashuka dimbani Oktoba 22 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons
ADVERTISE HERE