Kiungo bora zaidi nchini Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' amewakata ngebe mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiamini fundi huyo atajiunga na timu yao
Katika moja ya mahojiano yake, Chama amesema ataongeza mkataba kuendelea kuwatumikia mabingwa wa nchi Simba
Kwa hapa nchini hafikirii kuitumikia timu nyingine kwani anaamini maisha mazuri yapo Simba tu
"Bado sijasaini mkataba mpya lakini natarajia hivi karibuni mambo yatakuwa sawa," alisema
Shabiki wa Yanga akamkaribisha ajiunge na timu yao lakini akampa jibu lililomkata maini kabisa!
"Asante sana, lakini hapa Simba pana raha zaidi patamu eeeh"
Chama ana mkataba na klabu ya Simba mpaka mwezi Mwezi Julai 2021, tayari mazungumzo yanafanyika ili kumuongeza mkataba
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ametaka nyota huyo apewe mkataba mpya mapema akihofia anaweza kuondoka mwezi Julai kwani ana uhakika timu kubwa barani Afrika zitajitosa kumuwania