Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre amewapongeza wachezaji wake baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa jana kwenye uwanja wa Taifa.
Akizungumza na wachezaji baada ya mchezo, Lechantre amesema ushindi dhidi ya Azam FC unaiweka Simba katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kama itaendelea na mwendo wake wa sasa.
Hata hivyo amewatahadharisha kuwa huu sio wakati wa kubweteka na kufikiria ubingwa kwani bado kuna michezo mingi.
Amesema anataka kuona wanapambana kwenye kila mchezo.
Simba imeshinda michezo sita mfululizo na iko kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 41, alama saba mbele ya Yanga iliyo nafasi ya pili.
Simba sasa inahamishia nguvu zake kwenye michuano ya kombe la Shirikisho ikitarajiwa kuivaa Gendarmarie ya Djibout kwenye mchezo wa awali siku ya Jumapili Februari 11 kwenye uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE