Majukumu Simba yamkwamisha Morrison Kamati ya Maadili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Oct 2020
Majukumu Simba yamkwamisha Morrison Kamati ya Maadili

Kamati ya Maadili ya TFF imeshindwa kutoa uamuzi juu ya shtaka la kimaadili linalomuhusu kiungo wa Simba, Bernard Morrison, baada ya mchezaji huyo kutoa udhuru na kushindwa kufika kwenye kamati hiyo akieleza kukabiliwa na majukumu ya klabu yake ya Simba

Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Kichere Mwita Waissaka amesema Morrison alituma wawakilishi ambao ni mawakili wake, lakini kutokana na uzito wa shauri lenyewe, kamati inamuhitaji mlalamikiwa mwenyewe badala ya wawakilishi ambao wasingeweza kujibu baadhi ya maswali.

"Kamati iliona kwamba kuna maswala yanatakiwa kujibiwa na yeye mwenyewe badala ya wawakilishi, kwahiyo suala lake liliahirishwa", amesema Kichere.

Morrison anakabiliwa na shtaka la kudharau kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kwa kitendo chake cha kusaini mkataba na Simba wakati shauri lake dhidi ya Yanga kuhusu mkataba wake likiwa bado halijaamuliwa.

Kuhusu rufaa ya Yanga kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS), Kichere amesema rufaa hiyo haihusiani na shauri lililopelekewa kwenye kamati hiyo, kwani rufaa ya Yanga inahusu usajili wakati shauri lililo mbele yao linahusu maadili.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’