Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara, amewahakikishia mashabiki watakaofika uwanja wa Azam Complex kushuhudia mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Ndanda Fc hawatajuta
Manara amewataka mashabiki wamiminike kwa wingi Azam Complex kushuhudia burudani na pira la levo za Kimataifa
Mchezo dhidi ya Ndanda utapigwa kuanzia saa 11:00 jioni.
"Wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani kuanzia wale wa makazi ya Chamazi, Kigamboni, Mbagala wanapaswa watambue kwamba mabingwa wa nchi Simba watashuka uwanjani kucheza dhidi ya Ndanda FC.
"Mechi hii ukiikosa utajitakia magonjwa kwani tutapiga mpira wa visukarisukari na ni uwanja mzuri tunakwenda kucheza sasa sijui unahitaji nini sasa hapo.
"Najua mnatambua kwamba kuna wachezaji wengi wazuri ndani ya Simba hivyo hakuna ambaye hajui namna timu yetu inavyofanya muda wote uwanjani," amesema.