Rweyemamu awachambua Miquissone, Morrison

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Oct 2020
Rweyemamu awachambua Miquissone, Morrison

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amewaelezea Luis Miquissone raia wa Msumbuji na Mghana Benard Morrison kuwa licha kuwa na vipaji vikubwa kwenye kusakata soka, lakini kuna kitu kikubwa kinachowatofautisha ambacho ni tabia zao

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa klabu hiyo, Patrick Rweyemamu baada ya mazoezi ya utimamu wa mwili 'gym', alisema pamoja na wote kuwa mahiri kwenye kusakata kambumbu, lakini Miquissone yeye kitabia ni mpole sana na si mtu wa kujichanganya kama mwenzake Morrison ambaye ni mcheshi.

"Luis ni mtulivu, si mchangamfu sana, siyo mtu wa kujichanganya sana, nadhani maisha aliyokulia hayakuwa ya kujichanganya, pia inaonekana ndiyo hulka yake." alisema meneja huyo na kumwelezea Morrison kuwa yupo tofauti na mwenzake.

"Yeye Morrison ni mtu wa kujichanganya, mcheshi, kila tukio yupo, pia ni mchekeshaji yaani 'komediani', na hii inasababisha maisha ya kambi yawe rahisi kwa wenzake na watu wengine kwa ujumla," alisema meneja huyo.

Miquissone alisajiliwa na Simba katikati ya msimu uliopita wa Ligi Kuu, kipindi cha dirisha dogo akitokea UD Songo ya Msumbiji alikokuwa akicheza kwa mkopo kutoka Mamelodi Sundowns, huku Morrison akisajiliwa usajili wa dirisha kubwa baada ya kumaliza mkataba na Yanga

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’