Kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla amesema kuwa hana hofu yoyote ile ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa nchi kwani bado anaamini ana nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa uwezo anao.
Ndemla ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kikosi cha Stars ambacho leo kinashuka dimba la Mkapa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi.
Kiwango cha juu alichoonyesha katika mechi tatu alizocheza kwenye ligi msimu huu, kimemshawishi kocha wa Stars Etienne Ndayiragije kumjumuisha kwenye timu yake
Nyota huyo aliyeitumikia Simba kwa takribani misimu nane, amesema anaamini nafasi ya kucheza pale Simba bado anayo
"Uwezo ninao na kikubwa ambacho kitanifanya niweze kufikia malengo niliyojiwekea ni juhudi pamoja na kujituma sina mashaka katika hilo," alisema
Ndemla aliongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia machampioni hao wa taifa hili kwa misimu mitatu mfululizo