Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Uganda, Emanuel Okwi huwa habahatishi anapocheza kwenye dimba la Taifa pamoja na uwanja wa Uhuru.
Bao lake pekee alilofunga dhidi ya Azam FC linamfanya afikishe mabao 13 akiongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.
Mabao yote 13 ameyafunga katika viwanja hivyo viwili hivyo kumfanya awe na rekodi ya kipee.
Aidha ushindi dhidi ya Azam FC ulisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba hasa ikizingatiwa katika michuano ya kombe la Mapinduzi, Azam iliifunga Simba huku zikitoka suluhu kwenye mchezo wa duru ya kwanza ligi kuu ya Vodacom.
Dalili za Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma kupata ushindi zilionekana mapema tu mchezo huo ulipoanza kutokana na mashambulizi yake mfululizo langoni mwa wapinzani.
Azam FC walizidiwa katika safu ya kiungo na kujikuta wanawapa fursa Simba kutawala mchezo sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza.

ADVERTISE HERE