Kuna kundi la Wanahabari kupitia kurasa zao za Mitandao ya kijamii wanamshambulia na kumkosoa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara
Ni kama vile kuna kikundi flani cha Wanahabari wamepewa kazi maalum ya kuhakikisha wanamtoa Manara kwenye 'reli' na pengine kumuharibia nafasi yake ndani ya klabu ya Simba
Sioni kama jambo hili litaweza kufanikiwa kwani Manara ndani ya klabu ya Simba, amejijengea mizizi
Umaarufu alioupata Manara Simba haukuja wenyewe tu, bali ni matunda ya kazi aliyoifanya kwa zaidi ya miaka sita
Wanasimba wanampenda Manara si kwa sababu nyingine, ni kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya uhamasishaji
Misimu minne nyuma, hamasa ndani ya klabu ya Simba ilikuwa chini sana, Manara alihusika kwa kiasi kikubwa kuifanya brand ya Simba ifike mahali ambapo ipo sasa
Kinachofanywa na kikundi hicho cha watu ni kampeni chafu ya kumshusha Manara, wakiamini wanaweza kumuondolea umaarufu wake na pengine kumfanya aondolewe katika nafasi yake
Hii ni kama ndoto ya mchana kwani Manara ni Simba na sidhani kama uongozi wa mabingwa hao wa nchi wanaweza kuzikubali propaganda zinazofanywa dhidi ya mtu wao muhimu sana linapokuja jambo la kuitangaza 'brand' ya Simba