Timu ya Taifa inaendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Burundi ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Nyota sita wa kikosi cha Simba ni sehemu ya wachezaji wanaotarajiwa kushiriki kwenye mchezo huo ambao uko katika kalenda ya FIFA
Picha juu 'vijana wa Matola' wakiwa katika majukumu hayo ya Kitaifa
Jana kocha Etienne Ndayiragije alimuengua nahodha msaidizi wa kikosi hicho John Bocco ambaye bado hajaimarika sawa sawa kutokana na majeruhi aliyopata mwezi uliopita
Nyota wa Simba waliobaki kwenye kikosi kuelekea mchezo huo ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Said Ndemla na Mzamiru Yassin
ADVERTISE HERE