Simba yapiga hesabu kali Ligi ya Mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Oct 2020
Simba yapiga hesabu kali Ligi ya Mabingwa

Klabu ya Simba imesema kuwa kwa sasa haina presha yoyote ile kwani wamekipata kile walichokuwa wakikisaka kwa takribani misimu saba

Tangu Simba ilipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2011/12, mabingwa hao wa nchi walilazimika kusubiri misimu mitano kabla ya kulishinda kombe hilo

Wekundu wa Msimbazi walirejesha ubabe wao msimu wa 2017/2018 walipotwaa ubingwa wa ligi hiyo kabla ya kufanya hivyo misimu miwili zaidi, yaani 2018/19 na 2019/20.

Kwa sasa mashabiki na wanachama wa Simba wamekuwa wakitembea vifua mbele kutokana na mafanikio hayo ya kubeba kombe la Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo, lakini ikiwamo kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2019/2019.

Katika kuonyesha uongozi wa Simba usivyotaka masikhara, umetamba kuendelea kulibeba kombe hilo la Bara msimu huu, ikiwamo kufika nusu fainali au fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Hesabu kali zaidi ni kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambako wengi wanaamini ndiko mabingwa hao wa nchi watapata ushindani wa kweli kwani kwa ligi ya ndani ni kama hakuna wa kuisumbua Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’