Jumamosi ya Oktoba 10 mabingwa wa nchi Simba watashuka kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kupimana ubavu na Pan Africa katika mchezo wa kirafiki
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya mechi zinazofuata za ligi kuu, Oktoba 22 wakitarajiwa kumenyana na Prisons
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema mechi hizi zitawapa nafasi na kuwaweka sawa wachezaji wao ambao hawana majukumu ya timu za Taifa
Mchezo mwingine wa kirafiki utapigwa Oktoba 14 dhidi ya Mlandege Fc ya visiwani Zanzibar
Tayari wamchezaji wa Simba wamerejea mazoezini baada ya mapumziko ya siku mbili
ADVERTISE HERE