Wachezaji wa Simba ambao hawakuitwa timu za Taifa wamerejea kambini kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Oktoba 22 mkoani Rukwa
Aidha kabla ya mchezo huo Simba inatarajiwa kucheza mechi kadhaa za kirafiki
Mkuu wa Idara ya Habari klabu ya Simba Haji Manara amesema watatumia kipindi hiki cha mapumziko ya mechi za Kimataifa kuwaimarisha wachezaji wao waliobaki
"Timu inajiandaa na mechi nyingine za ligi hasa baada ya mchezo wetu wa dabi dhidi ya Yanga kupelekwa mbele sisi hatuna cha kusema katika hilo kazi yetu ni kucheza.
"Kwa namna ambavyo tumejipanga tutacheza mechi mbili za kirafiki ambapo moja itakuwa ni Oktoba 10 tutacheza mechi ya kirafiki na Pan Africa halafu baadaye tutacheza mechi nyingine na Mlandege.
"Tunaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi nyingine na timu ipo tayari kwa ajili ya kupambana masuala ya ratiba wenye mamlaka wanajua namna ya kupanga," amesema Manara