Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kuwa kwa namna kikosi chake kilivyo huwa anapata tabu kuchagua kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wa kila mchezaji ndani ya uwanja na wakiwa mazoezini.
Baadhi ya wachezaji wenye ywezo mkubwa lakini kwa sasa wanakosa nafasi Simba ni pamoja na Francis Kahata, Hassan Dilunga, Miraji Athumani, Ibrahim Ajibu, Bernard Morrisons, Erasto Nyoni na Beno Kakolanya
Sven amekiri kuwa amekuwa akipata wakati mgumu kwenye kuchagua kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wa wachezaji wake.
"Ukitazama kwenye kila idara kwangu kuna wachezaji zaidi ya wanne, labda kwa mfano ukigusa upande wa washambuliaji ninao wanne ambao ni Meddie Kagere, Charlse Ilanfya, Chris Mugalu na John Bocco.
"Kila mchezaji ana uwezo na kila mchezaji anahitaji kucheza, hakuna chaguo na huwezi kuwatumia wote hivyo kwangu ni furaha kwa kuwa ninakuwa kwenye wakati mgumu huku nikiwa na wachezaji ambao wanauwezo wa kunipa matokeo.
"Kinachotakiwa ni kwa kila mmoja kupambana ndani ya uwanja ili kuonyesha uwezo zaidi ya mwingine na ninaamini wote ni bora na nitawatumia," amesema
Kwenye mechi tano ambazo amekaa kwenye benchi ameshuhudia wachezaji wake wakifunga mabao 14 na Aishi Manula mlinda mlango namba moja akiokota mipira nyavuni mara mbili tu